Header Ads

Na James Timber, Mwanza Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela kupitia Mradi wa Shirika la Plan International Mkoa wa Mwanza, imekadidhi baiskeli 72 kwa wawakilishi wa jamii zenye thamani ya shilingi 15,840,000/= kwa lengo la kurahisisha huduma ya mawasiliano kwa wanajamii na familia zinazoishi mbali. Akizungumza wakati akikabidhi baiskeli hizo kwa Niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Afisa Tawala Wilaya ya Ilemela Neema Kipeja, ametumia fursa hiyo kuwapongeza Shirika la Plan International kwa kujitokeza kwenye jamii pamoja na kushirikiana na serikali kwa kutoa misaada mbalimbali ikiwemo usaidizi wa ujenzi wa madarasa pamoja na kugawa vifaa vya kujifunzia mashuleni, ambapo ameeleza ushiriki wao katika ngazi ya Kata umeleta mafanikio chanya kama kushiriki na jamii kwenye ujenzi wa majengo kwa baadhi ya vituo vya afya. Naye Meneja wa Shirika la Plan International Mkoa wa Mwanza, Baraka Mgohamwenda, amesema jumla ya Baiskeli 72 zimekabidhiwa kwa wanajamii wa kujitolea, wengine 86 waliapata baiskeli hizo katika utekelezaji wa miradi mbalimbali iliyopita, na kufafanua kuwa kutokana usafiri huo uliotolewa utasaidia wadau kukusanya taarifa za uhakika moja kwa moja na kupeleka mawasiliano hayo katika ofisi za plan kutoka kata zilizopo vijijini ambapo maeneo hayo usafiri wa Pikipiki na gari haupitiki kirahisi isipokuwa baiskeli. "Jamii kubwa ambayo tunaifanyia kazi ni ile ambayo inaishi mazingira duni na ambao tunaamini wengi wao wapo maeneo ya vijijini, mfano kule Kata ya Sangabuye nyumba ziliezuliwa kwa upepo na taarifa tulizipata kutoka wa mwakilishi wa jamii ambaye yupo maeneo hayo nasi pia tulifika haraka na mambo yalienda vyema, alisema Mgohamwenda Naye mmoja kati ya mwakilishi wa jamii Safari Joseph kutoka katika Kata ya Sangabuye, amelishukuru shirika hilo kwa kwa kumpa baskeli hiyo na kuahidi kuendelea kufanya kazi yake kifanisi zaidi tofauti na hapo awali alipokuwa akitembea mwendo mrefu sehemu ambazo ni hatarishi kwa ajili ya kukusanya taarifa. "Nilianza kazi na Plan International tangu mwaka 2002 na baadhi ya vijana ambao walikuwa wanaishi maisha duni katani kwangu nilitoa taarifa zao katika shirika la Plan, ambapo kwa sasa baadhi yao wamemaliza elimu ya sekondari na wengine wameajiriwa katika sekta binafsi na serikali, yote hayo ni mafanikio ya Plan, kutokana na usafiri huu naimani nitafanya kazi zaidi ya hapo, alisema.

by Thursday, November 22, 2018
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela kupitia Mradi wa Shirika la Plan International Mkoa wa Mwanza, imekadidhi baiskeli 72 kwa wawakilishi w...Read More
Powered by Blogger.