Header Ads

https://www.youtube.com/channel/UCERjz5nmYNOtG_WBi-1S4xA

Mahojiano na Aliyenusurika Katika Shambulio Lililoua Askari WanneKwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba anasema tukio limeondoa maisha ya askari wanne na kujeruhi raia wawili.

Majeruhi mmoja anaitwa Ally Chionda ambaye ni mfanyabiashara wa duka la vifaa vya ujenzi karibu na benki ya CRDB ambayo pilisi wamepoteza maisha.

Anadai walikuja majambazi kwenye muda kama wa saa 1:15 usiku wakiwa na pikipiki kama tano na kila pikipiki ilikuwa na watu wawili.

Kulikuwa na watu sita au saba ambao walikuwa wamebeba bunduki.

Walipofika walianza kupiga risasi upande wa eneo la benki na upande wa duka lake.

Bahati mbaya risasi moja ilimpata kwenye mguu wa kushoto ikatokeza na kwenda tena kwenye mguu wa kulia.

Majeruhi anaendelea vizuri na anategemea kufanyiwa x-ray kwa uchunguzi zaidi

No comments:

Powered by Blogger.