Header Ads

https://www.youtube.com/channel/UCERjz5nmYNOtG_WBi-1S4xA

NANI KUIBUKA 'SUPASTAA' WA SINGELI MBAGALA, CHAMAZI?


Image result for MIC PICTURE
Na Nasri Bakari 0713 311 300
Kampuni kubwa ya burudani Tanzania, Quality production, imeamua kuleta burudani kwa wakazi wa Chamazi na viunga vyake, ambapo itasaka vipaji mbalimbali kama vile   kucheza,kuigiza na kuimba muziki maarufu unaopendwa kwa sasa Tanzania, singeli.


   Akizungumza na mtandao huu, mratibu wa shindano hilo, Yahya Masangula alisema dhumuni la      kuandaa mashindano hayo ni kupata vipaji na kuvikuza na washindi watakaofanya vizuri watajipatia zawadi nono pamoja na kusimamiwa kazi zao.


“Tumeamua kuanzisha mashindano haya kwa lengo la kutambua vipaji vya wakazi wa Chamazi na maeneo ya karibu  na washindi kwenye kila kipengele watapata zawadi na kusimamiwa kazi zao,  hatimaye kufanikiwa kimuziki."


"tunarajia kuanza mashindano hayo, Septemba 16,2016, katika ukumbi wa Mashi Pub uliopo Chamazi, Magengeni na form zinapatikana Songa Art,Alhaji Barber Shop,Mbande na ofisi za Tamaduni, Chamazi,Magangeni kwa mawasiliano zaidi tupigie simu namba 0718 123552, 0655537372 au 0742 532203,” alisema Masangula.

Pia, alisema kila form inapatikana kwa bei ya shillingI 5000 na kwa waimbaji ni mtu mmoja mmoja, kucheza ni  kikundi cha watu wasiozidi watano na kuigiza ni mtu  mmoja mmoja au kikundi.
No comments:

Powered by Blogger.