Powered by Blogger.
[4] [Tech] [slider-top] [Technology]

Latest Post

HABARI KALI ZA WIKI

[15] [recent] [slider-top] [HABARI KALI ZA WIKI]

Technology

Lifestyle

HABARI ZA BURUDANI

[4] [burudani] [recent] [HABARI ZA BURUDANI]

Sports

VIDEO KALI ZA WIKI

NEW SONG:DIAMOND FT A,K,A

Gallery

Random Posts

Business

Boss Ngasa

Boss Ngasa

Video Of Day

STORI KALI ZA WIKI

[5] [habarimbalimbali] [recent] [STORI KALI ZA WIKI]

Popular Posts

Pages

STAY CONNECTED

[10] [recent] [slider-top-big] [HABARI KALI ZA WIKI]

CONTACT US

SIASA

[4] [siasa] [recent] [HABARI ZA SIASA]

Flicker Images

TUMA UDAKU PICHA AU VIDEO KUPITIA 0716909567

Facebook

About US

Advertisements

Entertainment

Follow US

You are here: Home / Ndege moja kati ya mbili za ATCL Alizonunua Rais Magufuli Itatua Kesho Nchini

Ndege moja kati ya mbili za ATCL Alizonunua Rais Magufuli Itatua Kesho Nchini

| No comment


Ndege ya kwanza kati ya mbili zilizonunuliwa na Serikali za Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), inatarajiwa kuingia  nchini kesho ikitokea Canada.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam jana na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL, Patrick Itule alisema ndege hiyo aina ya Bombardier Q400 inatarajiwa kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 7:00 mchana.

Itule alisema ndege hiyo yenye uwezo wa kubeba abiria 76, tayari imeanza safari ya kuja nchini tangu mwishoni mwa wiki iliyopita ikipitia miji ya Reykjavík, Southampton, Malta, Luxor, Addis Ababa Ethiopia kabla ya kutua nchini ikiwa na timu ya marubani wanne kutoka Canada.

“Ndege ya pili inatarajiwa kukabidhiwa Septemba 22 na kuanza safari ya kuja Tanzania Septemba 23,’’ alibainisha.