Header Ads

https://www.youtube.com/channel/UCERjz5nmYNOtG_WBi-1S4xA

NDEGE ZA MAGUFULI ZAANZA KUWASILIatc

Ndege ya kwanza kati ya mbili zilizoagizwa na serikali, aina ya Bombadier Q400 kutoka nchini Canada tayari imewasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere uliopo jijini Dar es Salaam.


Ndege hizi mbili zimenunuliwa kulifufua shirika la ndege la Tanzania (ATCL) ambalo kwa sasa lina ndege mbili, ambayo moja ni ya kukodi. Ujio wa ndege hizi mbili umeelezwa kuwa umelenga kusaidia katika soko la ndani, na kusaidia kurahisisha usafiri wa anga kwenda maeneo mbalimbali ya Tanzania.whatsapp-image-2016-09-20-at-1-09-15-pmNdege mpya ya serikali, Bombardier Q400 ikiwa katika uwanja wa Dar es Salaam mchana huu

Ndege hizi zitakuwa na uwezo wa kutua katika viwanja vingi nchini kwani huhitaji takribani barabara ya urefu wa kilomita 1 tu kuweza kuruka tofauti na ndege zinazotumia jet engine ambazo huhitaji zaidi ya barabara yenye urefu wa kilomita 2 kuweza kuruka.
Tunaendelea kuweka picha zaidi katika ukurasa huu hii leo baada ya waandishi kuruhusiwa kuingia ndani.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.