Header Ads

https://www.youtube.com/channel/UCERjz5nmYNOtG_WBi-1S4xA

RAMSEY NOUAH: NILIKUWA OMBAOMBA


Ramsey Nouah; NILIKUWA OMBAOMBA 
Tumeshawahi kusikia visa vya kuhuzunusha vya wasanii wakubwa hapa nchini kama Diamond Platinumz na wengineo, maisha yao ya nyuma yalivyokuwa ya kusikitisha na kukatisha tamaa. Hata hivyo pia kuna wasanii wakubwa na nguli barani Afrika waliopitia njia kama za akina Diamond.
Anaweza akawa staa wa muvi ambaye ameiteka Afrika, unamkubali na anayekuvutia sana, lakini hutaamini maisha yake ya nyuma yalivyokuwa ya kuogofya na kusikitisha sana.
Kisa cha msoto wa maisha ya kuishi chini ya madaraja na kuwa ombaomba katika jiji la Lagos  chini Nigeria aliyokutana nayo mwigizaji maarufu barani Afrika Ramsey Nouah akiwa na mama yake inaweza kuamsha wale ambao wamekata tamaa na hawana tumaini tena baada ya kuwa katika hali duni ya kiuchumi au vinginevyo.
Akihojiwa na jarida la Stargist Ramsey anayetambulia zaidi kama ‘lover boy wa Nollwood’ alisema safari yake ya kimafanikio imonyesha kweli katika maisha hakuna njia ya mkato ‘shotikati’ bali ni kupiga mzigo kwa bidii na matamanio ya kufanikiwa.
“Niliishi mitaani ambapo mimi na mama yangu tulilala vichochoroni, tulitandika kijimkeka ambacho ilitulazimu kujibana ili kutosha kulala wote wawili. 
“Wakati huo mama hakuwa katika hali nzuri, hatukuwa na kitu. Hatukuwa na pa kuishi, pia hatukuwa hata na kikombe cha maji ya kunywa, mama aliomba kila kitu hadi majiko ya kupikia.
“Wakati huo siwezi kuusahau maishani, wakati mbaya kabisa, hatukuwa na kitu, ilifika muda tuapitisha siku tatu au nne hatujala. Una njaa tumbo linanguruma lakini cha kusikitisha unakuwa huna cha kufanya wala pakwenda.
Baba huyo mwenye watoto wawili aliedelea “Ni bahati mbaya sana hakukuwa na mtu akiturekodi labda ningeweza kuwaonyesha hapa. Kwa kweli namshukuru sana Mungu kwa hapa nilipo. Kwa wakati huo nikitaabika nilimchukia kila mtu, nilikuwa najiuliza kwa nini Mungu ananifayia hivi? kwanini mimi?. Lakini nashukuru Mungu alikuwa na makusudi yake kwamba alihitaji nipitie maisha ya aina ile ndipo nije kuwa mimi kama nilivyo. 
Ramsey

No comments:

Powered by Blogger.