Header Ads

https://www.youtube.com/channel/UCERjz5nmYNOtG_WBi-1S4xA

Shilole: Sitaacha Kutoka na Serengeti boys, Mniache na Maisha yangu


Mwanamuziki wa Bongo flava asieishiwa vimbwanga mitandao kwa skendo ya kutoka na vijana wadogo walio chini ya umri wake(Serengeti Boys) amefunguka na kusema asipangiwe ni nani wa kuwa naye na ataendelea kutoka na viboi vyake.

Akiongea mbele ya Camera za eNewz, Shilole amesema mashabiki wanahitaji yeye awe na mzee lakini yeye haoni haja ya kuwa na mzee kwa kuwa hawawezi ‘kumpetipeti’ na kuwataka wamuache achague anachotaka kwa vile nyumbani yeye ni Zuwena na jukwaani ni Shilole.

“This is my life, nikiwa nyumbani ni Zuwena na nikiwa kwenye TV ni Shihi, maisha yangu mimi ya nyumbani au maisha yangu binafsi wao yasiwahusu sana ninaangalia upendo wangu upo wapi.

Nikisema niangalia mashabiki nini wanacho taka wao wanataka niwe na mzee, sasa maisha yangu nianze kuwa na mzee nianze kumburuza! mimi ninahitaji kijana aanze kunipetipeti” Alifunguka Shilole kwa madaha.

Lakini Shilole alimalizia kwa kusema kuwa mpenzi wake mpya wa sasa ni msanii wa muziki na wala hajawahi kubahatika kuwa na mpenzi ambaye ni dakitari au mwalimu, bali ana nyota ya kukutana na wasanii tu.

Akifafanua zaidi kwenye muonekano wake katika video ya Rayvan, Shilole amesema hakuvaa chochote ndani(chupi) zaidi ya ‘night dress’, hivyo ilimbidi atupie kileo ili aweze kufanya scene hiyo.

No comments:

Powered by Blogger.