Header Ads

https://www.youtube.com/channel/UCERjz5nmYNOtG_WBi-1S4xA

Alikiba Ana Mziki Mzuri Lakini Kuna Walakini Mahali...Hivi Hana Timu ya Kuhakikisha Kila Kitu Kipo Sawa?


Ule usemi wa kwenye miti hakuna wajenzi nimeliona kwenye hiyo Show ya Mombasa hasa baada ya Ali Kiba kuhojiwa na kipindi cha Mseto... kwa kweli huyu msanii anahitaji Management. Anajisikia sana anategemea mashabiki sana anasahau hata mitume walisalitiwa na watu "Eti sallam alikuwa backstage" Swali la kujiuliza hapo timu yake ilikuwa inafanya nini mpaka Sallam Akafanya yake kuzima mziki?

Huyu jamaa hayupo kibiashara amejidhalilisha sana kwa kuonyesha team ya Diamond ipo vizuri sana kiasi cha kumdhalilisha. Hivi huyo msanii wa Marekani na Alikiba mbona wapo sawa tu? Hakupaswa kurudi jukwaani kuimba.

Ni muda umefika akapata management amabayo inajua ataongea nini atavaa nini alale wapi. Na kama anayo management awafute kazi. Nadhani Alikiba anahitaji msaada haiwezekani aende Kenya bila mtu backstage.

By Pascal Ndege

No comments:

Powered by Blogger.