Header Ads

https://www.youtube.com/channel/UCERjz5nmYNOtG_WBi-1S4xA

AUDIO: Wanafunzi waliodaiwa kulawitiwa Moshi wafikia 35, wazazi wazungumza

Siku kadhaa zimetolewa taarifa kuwa baadhi ya watoto wa kiume katika shule ya msingi Kaloleni iliyopomo Moshi Mkoanu Kilimanjaro wamelawitiwa na wale wa kike kufanya mapenzi na watu waziama.
Imeelezwa kuwa idadi ya wanafunzi wa kiume wanaodaiwa kulawitiwa na wa kike kufanya mapenzi wakiwa katika umri mdogo pamoja na kubakwa katika shule ya msingi kaloleni imefikia 35 baada ya jeshi la polisi kuendelea kuwahoji pamoja na madaktari  kuwapima huku jeshi hilo likiwakamata watu 2.
Ripota wa millardayo.com na Ayo TV alimpata mama ambaye ana mwanafumzi anayesoma shuleni hapo nakusema hata yeye alishapata taarifa za mtoto wake wa kiume kufanya vitendo hivyo na inaelezwa  wanafunzi hao walikuwa wanapewa fedha kuanzia shilingi 500 ili wasitoe taarifa. 
Kamanda wa polisi kilimanjaro Wilbroad Mutafungwa  amesema  uchunguzi bado unaendelea na tukio hilo liligunduliwa na walimu wakati wakiwahoji wanafunzi hao baada ya maendeleo ya taaluma kushuka huku kamanda akisema tatizo hilo mara nyingi limekuwa likitokea baada ya wazazi kutofuatilia mwenendo wa wanafunzi wao.
Full stori ipo hapa, Bonyeza play

No comments:

Powered by Blogger.