Header Ads

https://www.youtube.com/channel/UCERjz5nmYNOtG_WBi-1S4xA

Diamond Aanza Mazoezi ya Kuimba Live na Band Kama Ali Kiba...Show za Uingereza na Neyo Atazipiga na Band


Mwanamuziki Diamond Platnumz ameweka picha kwenye ukurasa wake wa Instagram zikionyesha akifanya mazoezi ya uimbaji akiwa na bendi yake ya muziki akieleza kuwa anajiandaa kwa ajili ya matamasha yake (music tour) yanayokuja hivi karibuni.

Diamond Platnumz anatarajia kufanya ‘tour’ ya muziki nchini Uingereza akiwa na mwanamuziki Ne-Yo siku za karibuni. Lakini pia alisema kuwa maandalizi ya kuimba na bendi sio tu kwa ajili ya ‘tour’ hiyo kwani hata kwenye matamasha mengine atakuwa akiimba ‘live’.

Aidha, alieleza kuwa alichelewa kuanza kutumia bendi kwa sababu alikuwa akitaka apate wapigaji vyombo wenye ujuzi. Unajua wakati mwingine unaweza ukawa unaimba na bendi lakini ukaonekana unaimba vibaya sababu ya upigaji mbaya wa vyombo, mimi sikutaka hilo ndio sababu ilinichukua muda ili nipate watu wazuri, alisema Diamond Platnumz.

No comments:

Powered by Blogger.