Header Ads

Mkubwa Fella Aweka Wazi Bifu Lake na Diamond


 fella3

BAADA ya hivi karibuni kudaiwa kuwa ana bifu na msanii wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, bosi wa Yamoto Band, Said Fella (pichani juu) amefunguka kuwa tetesi hizo siyo za kweli na haijawahi kutokea.
Habari kutoka kwa vyanzo mbalimbali zilidai kuwa wawili hao waliingia kwenye bifu baada ya wasanii wa Bendi ya Yamoto anayoisimamia kumlalamikia Diamond ambaye pia ana hisa kwenye bendi hiyo kwamba mkurugenzi wao huyo anawanyonya na kazi zote wanazopiga wao wanamnufaisha yeye tu!
diamond
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
Uwazi Showbiz lilipomtafuta alisema: “Hakuna kitu kama hicho na haijawahi kutokea kabisa, hayo ni maneno tu ya watu na wala mimi na Diamond hatujawahi kuzungumza kitu kama hicho.”

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.