Header Ads

https://www.youtube.com/channel/UCERjz5nmYNOtG_WBi-1S4xA

MKURUGENZI WA MANISPAA YA UBUNGO ATEMBELEA WODI NA KUZUNGUMZA NA WAFANYAKAZI HOSPITALI YA SINZA

MKURUGENZI WA MANISPAA YA UBUNGO MHESHIMIWA JOHN L. KAYOMBONa Nassir Bakari

Mkurugenzi wa Manispaa  ya Ubungo Mh .John L. Kayombo  ametembelea  na kukagua wodi mbalimbali za wagonjwa  na kuzungumza na wafanyakazi wa hospitali ya Sinza iliyopo Sinza Palestina.
    
Ziara hiyo ambayo imetokana na hatua ya Mkurugenzi  kutaka kufahamu kero za wafanyakazi na miundo mbinu ya utoaji huduma ya hospitalini hapo.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mkurugenzi alisema amesikitishwa na hali aliyokuta hapo ikiwemo uchakavu wa vitanda ,majengo pamoja na uhaba wa wataalamu wa idara mbalimbali.

“Kwa kweli  nimesikitishwa  na hali niliyokuta, inafika hatua mpaka vitanda vinakuwa chakavu namna hii?” alihoji  Mkurugenzi.

Wakati huo huo Mkurugenzi   ameahidi kufuatilia mapato katika hospitali hiyo kwa kuanzisha mfumo wa kieletroniki utakaosaidia kukusanya kwa uaminifu na umakini na kuzuia mianya ya wizi wa pesa.

“Nitaajiri watu wa Mifumo ya habari(IT), waje watufunge mitambo ya kielektroniki itakayopunguza mianya ya wizi wa pesa,” alisema Mkurugenzi Kayombo.

Pia alisikiliza kero  zinazowakabali  wafanyakazi wa idara mbalimbhali na kuahidi kuzitatua kwa wakati bila upendeleo wowote.

“Nimesikiliza kero zenu kwa umakini, naahidi kushughulikia  moja baada ya nyingine na nawakaribisha ofisini kwangu muda wowote na kama kuna mfanyakazi ana tatizo lolote asisiste kuniambia," alisema Mkurugenzi Kayombo.
Displaying IMG_20161008_191226.jpg
MKURUGENZI WA MANISPAA YA UBUNGO MH. JOHN L. KAYOMBO AKIANDIKA KERO NA MAONI YA WAFANYAKAZI WA HOSPITALI YA SINZA


Displaying IMG_20161008_191358.jpg
MKURUGENZI WA MANISPAA YA UBUNGO MH. JOHN L. KAYOMBO AKIMSALIMIA MGONJWA ALIPOTEMBELEA KATIKA WODI YA WAZAZI HOSPITALI YA SINZA.

Displaying IMG_20161008_191848.jpg
MKURUGENZI WA MANISPAA YA UBUNGO MH. JOHN L. KAYOMBO KATIKATI AKITOKA NJE YA UKUMBI WA MIKUTANO BAADA YA KUFANYA KIKAO NA WAFANYAKAZI WA HOSPITALI YA SINZA.

IMETOLEWA NA
NASSIR BAKARI
AFISA HABARI
MANISPAA UBUNGO
PHONE:0713 311 300

No comments:

Powered by Blogger.