Header Ads

Rais JPM Aongoza Waombolezaji, Viongozi Kumuaga Masaburi Dar


msiba
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli na mkewe wakitoa heshima zao za mwisho na kuaga mwili wa aliyewahi kuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Dk. Didas Masaburi katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar leo.
masaburi
Zoezi la kuaga mwili wa aliyewahi kuwa Meya wa Dar es Salaam, Dk. Didas Masaburi likiendelea katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar leo. 
1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli pamoja na viongozi wengine wakiwa katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar leo wakati wa kuaga mwili wa aliyewahi kuwa Meya wa Dar es Salaam, Dk. Didas Masaburi. 2
Sehemu ya wafiwa wakati wa kuaga mwili wa aliyewahi kuwa Meya wa Dar es Salaam, Dk. Didas Masaburi katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar leo.
Rais Dk. John Pombe Magufuli leo ameongoza waombolezaji na viongozi wa serikali na vyama vya siasa kuuaga mwili wa aliyekuwa Meya Mstaafu wa Jiji la Dar es Salaam, Dk. Didas Masaburi kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar.
Wakati akitoa salamu zake, Rais Magufuli amesema kuwa alimfahamu Dkt. Masaburi kama rafiki yake, ndugu yake, na mpiganaji mzuri wa Chama cha Mapinduzi, na kwamba ni mtu aliyefanya makubwa katika Jiji la Dar es Salaam.
Viongozi walioungana na Rais Magufuli katika kumuaga Masaburi ni pamoja na Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete, Mjumbe wa Kamati Kuu Chadema Edward Lowassa, Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana na Meya wa sasa wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.