Header Ads

https://www.youtube.com/channel/UCERjz5nmYNOtG_WBi-1S4xA

Stori Mpya Kuhusu Sababu ya Scorpion Kumtoboa Said Macho


Makala hii imeanza kuzunguka katika mitandao mbalimbali ya kijamii leo asubuhi ikielezwa kutoka kwa mkazi wa Buguruni anayesema anakifahamu vyema kisa cha Scorpion kumtoaboa macho mkazi wa Dar es Salaam aliyefahamika kwa jina la Said Ally.

Katika habari zilizotolewa na mhanga, alisema kuwa alikuwa akitokea kazini kuelekea nyumbani na alipokuwa akinunua mahitaji yake ya nyumbani eneo la Buguruni, ndipo alivamiwa na mtu huyu anayefahamika kama Scorpion na kumfanyia ukatili huo.

Hii hapa chini ndiyo stori mpya inayoeleza kwa upande mwingine sababu za tukio hilo.

Inaelekea wanaume wa mkoani hawamjui scorpion. Halafu sisi watu wa Buguruni tunamjua huyo Saidi na shughuli zake, na pia tunajua shighuli za Scorpion ndio maana watu hata hawakuhangaika nao.

Watu waliwaacha wamalize mambo yao.

Tunaangalia tu watu wanavyo shadadia mambo wasiyoyajua kwa undani wakipiga kelele dunia nzima ikiwa ni pamoja na mkuu wa kaya ya Jiji.

Scorpion ni mtu aliyeamua kujichukulia sheria mkononi kwa kuwa uwezo huo anao.
Kwa maana ya uwezo wa kupambana na mtu yoyote ambae ni mtukutu. Anapiga kareti kama za kwenye kideo na physic yake sio ya wanaume hata 2 wa kawaida. He is a man na nyongeza.

Kwa kifupi ni kwamba Buguruni kuna watu watanashati na wanashughuli zao za maana lakini wanamiliki mitandao ya vibaka ambao hupora na kuwaletea mizigo wanayopora.

Na hiyo ndio wanapopatia hela zao nyingi.

Hujawahi kujiuliza Tv, radio, vipochi, simu na vitu vingine kama hivyo vikiibiwa huwa vinaenda wapi?

Wale waibaji huenda na kumkabidhi mtu halafu wanapewa hela flani ndogo(ya kula).
Yeye huvitakatisha vile vitu kwa kuviuza kupitia legitimate channels kwa yeye hubaki kuwa mtu legit.

Scorpion alikua ametangaza kiama kwa vibaka pale Buguruni. Na alikua anawashughulikia kweli. Hivyo he was posing a danger kwenye biashara za watu.
Wakati vibaka wakindelea kushughulikiwa na hali ikionekana imeanza kuwa swari, yani vibaki waliosalia wanahamia kambi nyingine kama vingunguti, gomz etc.
Ndugu wa kike wa mpiga kareti (rafiki wa scorpion) akaporwa pochi iliyokua na simu maeneo ya Buguruni sheli.

Scorpion akaamua kumsaka muhusika na hakufanikiwa kumtambua. Akaamua kutuma ujumbe kwa mkuu wao ambae ndie mhanga wa macho, kuwa anataka arejeshewe mali iliyoporwa.

Kama kawaida ya wapanga misheni mkuu akapiga kimya.

So Scorpion akaamua kudeal nae, the boss himself ndio akamfuata alipomkuta and the rest of the story baada ya kumfuata face to face mtakua mmeipata kwenye media.

Sasa nyie mpeni mamilioni na assets bosi wa wahalifu kisa mnamhurumia wakati hamumjui.

Ndio maana watu hawakutaka kuingilia kesi wakati jamaa anasurubiwa. Sie wa buguruni tunaelewa.

Mtu hakurupuki tu kumtoboa toboa mtu asiyemjua.

No comments:

Powered by Blogger.