Header Ads

https://www.youtube.com/channel/UCERjz5nmYNOtG_WBi-1S4xA

AISEE SASA HII SIFA! DIAMOND KULA BATA NA AMBER ROSE CHRISTMAS

Na Sosy
MSANII wa bongo flava Diamond amabye kila siku jina lake linazidi kupasua anga za muziki wa kimataifa sasa aja na ujio wa part ya kula bata katika sikuu ya christmas na Amber rose kutoka majuu.

Katika kusherehekea Christmas mwaka huu, WCB wanatarajia kufanya show yao ya kwanza wakiwa pamoja, December 24 iliyopewa jina Wasafi Beach Party jijini Dar es Salaa.
Wasanii wote wa label hiyo wakiongozwa na Diamond watatumbuiza. Lakini huenda kukawa na ugeni mkubwa wa staa wa nje na tayari meneja wa Diamond, Sallam.
Akiweka picha ya mrembo wa Marekani, Amber Rose, Sallam ameandika kwenye Instagram, “Wangapi watu wanataka huyu dada ashuke bongo siku akinukishe watu wale nae Bata
Naye Diamond alichombeza kwenye post yake: Eti Manager @sallam_sk anauliza wangapi wangependa huyu dada @amberrose siku ashuke Bongo watu wale nae Bata???”
Huenda label hiyo ikawa imepanga kumleta mrembo huyo kuwa host wa tamasha lenyewe.
Hiyo haitakuwa mara ya kwanza kwa ex huyo wa Wiz Khalifa kuja Afrika. Mwaka jana alienda Lagos, Nigeria kwa mwaliko wa D’Banj ambako hata hivyo alikaa jukwaani kwa dakika 7 tu.

No comments:

Powered by Blogger.