Header Ads

Dogo Janja Kijana Aliyefaulu Kwa Maksi za Juu Somo la Kuanguka na Kuinuka

 

Msanii wa hop hop wa Kundi la Weusi, Nikki wa Pili amesema rapa kutoka Tip Top Connection, Dogo Janja ndiye msanii wake bora 2016. nikki-na-dogo-janja

Rapa huyo amedai Dogo Janja aliwahi kuteleza na kuanguka lakini ameweza kufanikiwa kuinuka katika kiwango cha juu mno huku akiwa na nidhamu ya hali ya juu na kuweza kufuta makosa yake.

“Abdul Kachaa aka Dogo Janja kijana mdogo aliyefaulu kwa maksi za juu somo lililowashinda mamilioni ya watu, wasomi, wafanyabiashara, wanamichezo,” Aliandika Nikki wa Pili Instagram. “Watu wa rika zote somo la kuanguka na kuinuka katika ubora wa kiwango cha juu, nidhamu, kufuta makosa yote,”

Aliongeza, “Show zake sasa zinaacha history, brand yake iko na professional look, confidence iliyovuka mipaka, kwa umri wake na aliyo ya fanya 2016. Namtangaza kuwa msanii wangu bora 2016,”

Dogo Janja ni mmoja kati ya wasanii wa hip hop waliofanya vizuri katika tamasha la fiesta lililofanyika Jumamosi hii katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es salaam.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.