Header Ads

dris Sultan aishia ‘Kula Kwa Macho’ Kwa Mrembo Sanchoka


Na Musa Mateja, Ijumaa
DAR ES SALAAM: Licha ya mbwembwe alizoonesha Mtangazaji wa Redio Choice FM, Idris Sultan katika kumtambulisha mwanadada Sanchoka anayedai ni mpenzi wake mpya baada ya kuachana na Wema Sepetu, inadaiwa jamaa huyo hajaona ‘ndani’ bado kwa mtoto huyo mzuri.

Rafiki wa karibu wa Idris aliyeomba hifadhi ya jina lake alilitonya Ijumaa kuwa, licha ya mshindi huyo wa BBA mwaka 2014 kumchombeza Sanchoka akitaka awe wake, bado hajaambulia kitu kwani modo huyo anaonekana kuwa si ‘maharage ya mbeya’.
“Ni kweli Idris alikutana na Sanchoka kule Sauzi kwenye Tuzo za MTV Africa (Mama) lakini alishia kula kwa macho tu, mtoto anaonekana kuwa na kamsimamo f’lani hivi na ndiyo maana licha ya kuvuma sana mpaka leo hajatia maguu Dar,” alidai mtoa ubuyu huyo.

Katika kubalansi habari hii Ijumaa lilifanya jitihada za kumtafuta Sanchoka kuzungumzia kilichopo kati yake na Idris lakini simu yake iliita bila kupokelewa.
Idris alipopatikana alisema kuwa, watu watasema mengi kama ilivyokuwa kipindi kile alipokuwa na Wema lakini ukweli ni kwamba ana malengo makubwa na modo huyo na si kwamba ana tamaa za kingono kwake.

“Watu wamekaa kingonongono tu, mimi nina future na yule mtoto na ikishakuwa hivyo kuna mambo lazima yasubiri, sasa wanaosema nakula kwa macho wao kinachowauma ni nini?” alihoji Idris.

GPL

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.