Header Ads

https://www.youtube.com/channel/UCERjz5nmYNOtG_WBi-1S4xA

HEKAHEKA: Mtoto asaka baba yake, asema aliambiwa ni msanii wa Bongo movie

Heka Heka ya Leo Tena ndani ya Clouds FM imekutana na mtoto ambaye alifika katika Studio za Clouds FM siku ya Ijumaa November 11 2016 na kukutana na Geah Habibu ambaye ameipata stori yake kuwa alifika hapo kwa lengo la kukutanishwa na baba yake mzazi ambaye ni msanii wa Bongo Movie aitwaye Cheki Budi.
http://i1.wp.com/www.bongomovies.com/wp-content/uploads/2016/05/Cheki-Budi.jpg?w=620

Heka Heka imezungumza na mama mzazi wa wa binti huyo ambaye ameeleza kuwa alikuja Dar es salaam kwa mara ya kwanza mwaka 2005 akiwa ni mke wa mtu na alikaa kwa siku 9 tu na wakati akikaribia kuondoka alienda Club ambako alikutana na mwanaume ambaye anatajwa kuwa ni Cheki Budi muigizaji wa Bongo Movie na ni siku hiyo hiyo alipata ujauzito.
>>>’Siku hiyo ambayo nilikwenda kwa huyo rafiki yangu ilikua siku ya Ijumaa akanambia twende nikupeleke Club leo  na akaniunganisha na huyo mwanaume kesho yake nikaenda kwake nikalala, keshokutwa yake nikaondoka kwenda Singida. Sasa kinachonishangaza ni nani kamwambia mwanangu kuwa baba yake ni huyo msanii wakati mimi sijawahi kumwambia’ – Mama Mtoto
>>>’Zena ndiye aliniuliza unamjua baba yako? mama ako ameshakuonesha baba yako? nikamwambia mimi simjui hilo ni suala gumu kamuulize mwenyewe, akasema nakupa siri usimwambie mama, baba ako ni Cheki Budi basi nikarudi nyumbani, siku moja nilimuuliza mama Clouds iko wapi naomba nioneshe nasikia kuna kituo cha watoto, mimi nataka nimuone tu Cheki Budi.’ – Mtoto
Stori kamili kuhusu mkasa huu bonyeza Play hapa chini kusikiliza.

No comments:

Powered by Blogger.