Header Ads

https://www.youtube.com/channel/UCERjz5nmYNOtG_WBi-1S4xA

HIZI NDIZO SABABU ZILIZOMFANYA WAZIRI MKUU WA DR CONGO KUJIUZULU MAPEMA


WAZIRI   mkuu nchini Jamhuri ya Demokrasi ya Congo Augustin Matata Ponyo, ameamua kujuuzulu mapema leo hii ili kuacha serikali ya mpito. 
Lakini pia amejuuzulu ili kutoa fursa kwa mrithi wake kuiongoza seriklai hiyo.

Kujiuzulu kwa bwana Ponyo ni sehemu ya makubaliano yaliyotiwa sahihi mwezi uliopita kati ya serikali ya Rais Joseph Kabila na baadhi ya vyama va upinzani ya kuhairisha uchaguzi wa urais hadi mwezi Aprili mwaka 2018.

Wapiga kura nchini DRC walistahii kupiga kura mwezi huu kumchagua mrithi wa Rais Kabila, wakati wa kumalizika kwa mhula wake wa mwisho.

Vyama vikuu vya upinzani vinakataa kuhairishwa kwa uchaguzi vikisema kuwa hiyo ni njama ya Rais Kabila ya kusalia madarakani.

Baraza lote la mawaziri lilijiuzulu na bwana Ponyo.
chanzo BBC Swahili

No comments:

Powered by Blogger.