Header Ads

HIZI NDIZO SABABU ZILIZOUFANYA MSAFARA WA MKUU WA MKOA WA LINDI KUZUILIWA PORINI

IMERIPOTIWA kuwa msfara wa Mkuu wa Mkoa wa Lindi umeshindwa kuendelea kwa muda  baada ya gari lilopata ajali kuzuiya msafara huo.
 Wakazi wa kata ya Kibata katika halmashauri ya wilaya ya Kilwa mkoani Lindi wameiomba Halmashauri hiyo kutatua tatizo la ubovu wa barabara inayounganisha kata hiyo na makao makuu ya wilaya kufuatia ubovu mkubwa wa barabara hiyo inayosababisha ajali za mara kwa mara hali inayokwamisha ukuaji wa uchumi kwa jamii.
screen-shot-2016-11-24-at-1-30-00-pm
Wakiongea na Channel ten kufuatia kutokea kwa ajali ya Lori lenye namba za usajili T 396 ACQ linalomilikiwa na Adam Mangosongo kulikochangiwa na ubovu wa barabara na kusababisha Kuzuia kwa masaa kadhaa msafara wa mkuu wa mkoa wa Lindi,Godfrey Zambi kabla ya kuinuliwa kwa ushirikiano wa wananchi wa kata hiyo.

Wakiongozwa na Mbunge wa jimbo la Kilwa kaskazini,Vedasto Ngombale Mwiru pamoja na wananchi wa kata hiyo wamebainisha kuwa kutokana na ubovu wa barabara hiyo ulazimika kupata huduma mbalimbali kupitia wilaya ya Rufiji Mkoani pwani.

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilayani ya kilwa,Zabron Bugingo ambae pia alishuhudia ajali hiyo alipotakiwa kutoa taarifa kuhusiana na barabara hiyo inayounganisha kata ya Kibata na Kata ya kipatimu wilayani kilwa pamoja Nyamwage wilayani Rufiji mkoani Pwani alieleza mipango ya ukarabati wa barabara hiyo.
SOURCE CHANNEL TEN

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.