Header Ads

https://www.youtube.com/channel/UCERjz5nmYNOtG_WBi-1S4xA

Kamanda Sirro Afunguka Kuhusu Wasiwasi wa Makonda kwa Jeshi la Polisi


Baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuonekana kuwa na shaka juu ya jeshi la polisi kwenye harakati za kutokomeza matumizi ya Shisha – Kamanda wa Polisi mkoa wa Dar es salaam Simon Sirro amefunguka juu ya tuhuma hizo.

Kamanda huyo amekiambia kipindi cha Sun Rise cha Times FM leo kuwa jeshi la polisi wanafanya kazi kwa mujibu wa Sheria na Operesheni ya kutokomeza Shisha jijini inaendelea kama kawaida kilicho baki ni mwanasheria mkuu wa serikali kuandaa mashtaka kwa watuhumiwa.

“Watu wamekamatwa ni wengi, kimsingi kazi inafanyika, sasa huo ni wasiwasi kama wasiwasi basi unabaki kuwa wasiwasi, kikubwa niseme tunafanya kazi kwa mujibu wa sheria na kanuni. Yeye ni Mwenyekiti wangu wa kamati ya ulinzi na usalama kwa hiyo ninaamini kama ana wasiwasi na chombo chake najua atakuja kutuita na kutuambia nini cha kufanya,” amesema Sirro.

“Lakini kama ana wasiwasi zaidi yeye ni kiongozi wetu atajua atachukua hatua gani dhidi yetu, kwa hiyo namuachia mkuu wangu wa kazi yeye ndio atajua nini cha kufanya.”

No comments:

Powered by Blogger.