Header Ads

Madee Ajibu Tuhuma Zinazomkabili Babu Tale Kuitelekeza Tip Top na Kumganda Diamond Platnumz


Msanii Madee ambaye ni miongoni mwa wasanii viongozi wa Tip Top inayosimamiwa na Babu Tale, amejibu tuhuma za meneja wao huyo kuitelekeza Tip Top na kuegemea zaidi kwa Diamond Platnumz.


Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Madee amesema hawezi kupinga maneno yaliyopo mtaani kwani ni kitu kinachoonekana kwao, lakini ukweli ni kwamba Babu Tale hajaitelekeza Tip Top, isipokuwa Diamond amekuwa na projects nyingi zinazohitaji uwepo wake kama meneja.
Hivi karibuni mashabiki wameibua hoja kuwa Babu Tale ameipotezea Tip Top na "kugandana" na Diamond, kwa sababu anafanya vizuri na safari za nje hazimuishi, kauli ambayo hata Niki Mbishi ameiimba kwenye wimbo wake wa Babu Talent.

Sikiliza sauti ya Madee akizungumzia suala hilo kwenye Planet Bongo ya East Africa Raio.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.