Powered by Blogger.
[4] [Tech] [slider-top] [Technology]

Latest Post

HABARI KALI ZA WIKI

[15] [recent] [slider-top] [HABARI KALI ZA WIKI]

Technology

Lifestyle

HABARI ZA BURUDANI

[4] [burudani] [recent] [HABARI ZA BURUDANI]

Sports

VIDEO KALI ZA WIKI

NEW SONG:DIAMOND FT A,K,A

Gallery

Random Posts

Business

Boss Ngasa

Boss Ngasa

Video Of Day

STORI KALI ZA WIKI

[5] [habarimbalimbali] [recent] [STORI KALI ZA WIKI]

Popular Posts

Pages

STAY CONNECTED

[10] [recent] [slider-top-big] [HABARI KALI ZA WIKI]

CONTACT US

SIASA

[4] [siasa] [recent] [HABARI ZA SIASA]

Flicker Images

TUMA UDAKU PICHA AU VIDEO KUPITIA 0716909567

Facebook

About US

Advertisements

Entertainment

Follow US

You are here: Home / MKE WA MAREHEMU MBUNGE WA LUDEWA AFUNGUKA LIKE NEVER BEFORE SOMA HAPA LIVE!!

MKE WA MAREHEMU MBUNGE WA LUDEWA AFUNGUKA LIKE NEVER BEFORE SOMA HAPA LIVE!!

| No comment
Ukiwa umepita mwaka mmoja tangu kifo cha aliyekuwa mbunge wa Ludewa (CCM), Deo Filikunjombe, mjane, wazazi na wakazi wa jimbo hilo wamefanya ibada ya kumkumbuka ambayo imeibua upya simanzi.

Filikunjombe alifariki dunia  Oktoba 15, 2015 katika ajali ya helikopta iliyoanguka na kulipuka katika Hifadhi ya Taifa ya Selous mkoani Morogoro wakati akitokea Dar es Salaam kwenda Ludewa  mkoani Njombe. Wengine waliokufa katika ajali hiyo ni Egid Nkwera (43), Casablanca Haule (53) na William Silaa, aliyekuwa rubani wa helikopta hiyo.

Akizungumza  wakati wa ibada hiyo, mjane huyo, Sarah alisema: “Huwa namuota mara kwa mara na hali hiyo inanifanya nizidi kumuombea kwa Mungu ampumzishe kwa amani.”

Aliishukuru familia ya marehemu kwa kuendelea kumpa mahitaji muhimu na kusomesha watoto.

Sarah ambaye wakati wa uhai wa mumewe alikuwa mama wa nyumbani, kwa sasa ameanzisha kilimo cha matunda na mbogamboga ili kuongeza kipato chake.

Philip Filikunjombe ambaye ni mdogo wa marehemu, amesema kifo cha kaka yake kimemuachia mzigo wa kutunza familia tatu ikiwamo yake na wazazi  wake (Deo).

Mbali ya kutunza familia hizo, pia anaendelea kusomesha zaidi ya watu 700 ambao walikuwa wakilipiwa ada na kaka yake wakati wa uhai wake.

Mkazi wa Ludewa, Ludende Mgimba alisema kifo cha Filikunjombe kilizima nuru ya maendeleo ya haraka aliyokuwa nayo kwa wakazi wa jimbo hilo.

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya wa Ludewa, Juma Madaha amesema anamkumbuka Filikunjombe kutokana na ujasiri na mapenzi aliyokuwa nao kwa wananchi wake.

Ibada hiyo ilifanyika Kanisa Katoliki la Ludewa kuanzia asubuhi na kufuatiwa na chakula cha mchana nyumbani kwa Filikunjombe, Mtaa wa Ibani.