Header Ads

https://www.youtube.com/channel/UCERjz5nmYNOtG_WBi-1S4xA

MREMBO TAMMY:AOMBWA RUSHWA YA NGONO ILI APATE SHOW


tammy (1)
WIKI hii tunaye msanii wa kike wa Muziki wa Hip Hop Bongo, Tamari Ally ‘Tammy the Baddest’ anayejulikana pia kama Nicki Minaj wa Bongo ambaye amepigwa maswali 10 na Mwandishi Wetu Andrew Carlos.

Unataka kujua kaulizwa nini akajibu vipi? Fuatilia hapa chini…
Ijumaa: Tukio gani huwezi kulisahau katika mapenzi?
Tammy: Nakumbuka nilikuwa natoka kimapenzi na msanii mwenzangu (jina linahifadhiwa). Alikuwa akijihusisha na uvutaji wa madawa ya kulevya sasa ndugu zangu wakawa wananishambulia kwa maneno kuwa napotea. Niliumia na kulia sana, kwa kuwa nilikuwa nampenda. Ila nilikuja kuachana naye.
Ijumaa: Hadi sasa umeshatoka kimapenzi na wasanii wangapi?
Tammy: Mmoja tu, baada ya kuachana na huyo wa awali niliapa sitakuja kutoka na msanii mwenzangu tena.
Ijumaa: Msanii gani Bongo unayetamani awe mpenzi wako?
Tammy: Duh! Kibongobongo wote nawachukulia kama kaka zangu tu.
Ijumaa: Unapenda kuvaa nguo za aina gani ukiwa na mpenzi wako faragha?
Tammy: Napenda kuvaa nguo laini zenye kumvutia bila kusahau bikini.
Ijumaa: Tunajua unatoka kimapenzi na mwanaume wa Nigeria, utamuamini vipi hawezi kukusaliti maana Tanzania na Nigeria ni mbali?
Tammy: Ujue wenzetu Nigeria wakitokea kumpenda mtu wanakuwa commited. Wanajali na kuthamini sana katika mapenzi. Huwezi kuwakuta wakisaliti hovyohovyo kama Bongo.
Ijumaa: Ikitokea sasa umemfumania mpenzi wako, utafanyaje?
Tammy: Sijui kwa kweli, nitaumia kama binadamu wengine. Kwa sasa mpenzi wangu ananiona ni kila kitu, maana akimtaka Beyonce ndiyo mimi, akimtaka Nicki Minaj ndiyo mimi ataenda wapi?
Ijumaa: Katika muziki wako ulishawahi kuombwa rushwa ya ngono?
Tammy: Ndiyo nilishawahi ila ilikuwa zamani sana. Nakumbuka ilikuwa shoo kubwa nikaombwa penzi na promoto mmoja ili nipewe shavu la kupafomu. Sikutaka ujinga huo, nikaachana naye na hata studio yao nikaihama.
Ijumaa: Inasemekana makalio yako ni ya Kichina hayafanani na Nicki Minaj orijino?
Tammy: Hapana jamani! Wabongo waliniita Nicki Minaj kwa sababu nimefanana naye na kipindi hicho nilikuwa na miaka 17. Kwetu tuna bahati ya kuwa na maumbo mazuri na makubwa mfano ukiwaona bibi zangu na mama yangu wote wameumbika.
Ijumaa: Ukiwa na mpenzi wako unapenda kumfanyia nini?
Tammy: Napenda kumpikia, kumfanya ajisikie yupo dunia tofauti.
Ijumaa: Tukio gani la muziki ambalo hutalisahau?
Tammy: Lilikuwa la kupanda jukwaa moja na staa wa Hip Hop wa kimataifa, Ludacris. Nakumbuka ilikuwa Fiesta ya mwaka 2012. Kingine ni pale Mwanamuziki AY aliponifuata na kuniambia kuwa alionana na staa wa Hip Hop Marekani, Tyga na kumwambia kuwa Tanzania kuna Nicki Minaj basi alishangaa sana na kusema ipo siku atakuja kuniona.

No comments:

Powered by Blogger.