Header Ads

SHILOLE ATANGAZA KUMNYOOSHA YEMI ALADE KWENYE JUKWAA LA FIESTA

Kuelekea November 5 kwenye kilele cha ule msimu wa Burudani Tanzania Fiesta 2016, mwanadada Shiloleameahidi kumfunika msanii wa kimataifa kutoka nchini Nigeria Yemi Alade kwa performance kali usiku huo.

Ni leo pande za THT wakati wasanii ambao wanatarajia kuperform kwa Live Band usiku huo walipokuwa wakifanya mazoezi ili kuhakikisha wanapiga show kali usiku huo.
Shilole alikuwa mmoja kati ya wasanii hao, ndipo informer wa Perfect255 akaona itakuwa poa kama akipiga nae story na kujua amejipanga vipi katika kutoa burudani usiku wa November 5 pande za Leaders Club.
“Mazoezi yako poa, nimejipanga kuingia na dancers zaidi ya 10 kwenye stage siku hiyo, nimeandaa surprises kibao kwa mashabiki wangu. Kama msanii lazima niwe na surprises za kutosha, kuna vitu vingi sana verry amazing. Miaka 3 iliyopita alikuja Yemi Alade lakini alinikimbia, sasa round hii kaja tena katika staje ya Fiesta namnyoosha.”
Hayo ni baadhi tu ya maneno ambayo Shilole alifunguka kuhusu alivyojipanga na show yake, kumsikiliza play hii video hapa chini.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.