Header Ads

https://www.youtube.com/channel/UCERjz5nmYNOtG_WBi-1S4xA

Tuzo Aliyonyang'anywa Wizkid yampa Alikiba umaarufu Nigeria


Mara tu baada ya EMA kueleza kinagaubaga jinsi walivyokosea kumpa Tuzo Wizkid badala ya Alikiba ,vyombo vya habari vya burudani nchini Nigeria vimemwelezea Alikiba kama msanii aliyepaswa kubeba tuzo ambayo Wizkid amechukua.

Kitu kilichoibua hoja zaidi ni baadhi ya mashabiki wa East Africa kuja juu na kudai kuwa msanii wao yuko vizuri kuliko Wizkid kitu ambacho kiliandikwa pia na vyombo vya habari huko ikiwemo magazeti, blog na redio...
Baadhi ya watu walionekana kushangaa lakini huku wengine walidai ni msanii aliyeko chini ya Sony.
Post ya Alikiba iliyoeleza uungwana wake kuhusu wanao mtukana Wizkid imeandikwa pia katika vyombo vya habari pia TV mbalimbali zimetoa habari hii.
Hapo karibuni kuna mitandao iliyoeleza uwepo wa msuguano baina ya Wizkid na Alikiba juu ya nani atangulie stejini na chombo hicho kimeeza kuwa hiyo ilipelekea kuchelewesha show lakini haikuwa proved kama ndivyo...

No comments:

Powered by Blogger.