Header Ads

https://www.youtube.com/channel/UCERjz5nmYNOtG_WBi-1S4xA

U HEARD: Kingine kilichomkuta Calisah baada video yake na Wema kuvuja


November 15, 2016 kwenye U Heard ya Clouds FM ipo na stori ya kuhusu kilichoendelea baada ya kuvuja kwa video ikiwaonesha mastaa Wema Sepetu na anayedaiwa alikua mpenzi wake, Mwanamitindo Calisah wakikiss.
Stori iliyopo leo hii inaeleza kuwa Calisah alikamatwa na Askari usiku wa kuamkia leo baada ya kwenda nyumbani kwa Wema Sepetu kuomba samahani baada ya kukiri kwake kwamba alivujisha video hiyo kutokana na hasira za kuachwa na Wema Sepetu ambaye ndiye alimzawadia simu aina ya iPhone 7 yenye thamani ya shilingi milioni 3.
Kwa mujibu wa Mchafu Chakoma inadaiwa Calisah alikwenda nyumbani kwa Wema Sepetu mitaa ya Ununio, Dar es salaam na kuanza kumuomba msahama bila kujua kwamba amewekewa mtego wa askari walioambiwa kwamba mwanamitindo huyo ana mpango wa kuendelea kuvujisha video na picha nyingine za kimapenzi walizowahi kupiga.
‘Amekamatwa jana usiku yuko Garden Polisi pale, alienda kwa bi mdashi kuomba msamaha, ishu ni mapicha mapicha mengi aliyosema anayo kwahiyo alikua anataka Kuyavujisha mengi tu kwenye mitandao kwahiyo ikabidi akamatwe kwa ajili ya kuzichukua hizo picha na kuzifuta, mimi sijaenda walienda askari, naskia bado yuko ndani’ – Mchafu Chakoma

No comments:

Powered by Blogger.