Header Ads

VIDEO: Kilichowakuta Wezi waliokuwa wakifukua makaburi…

Kenya ni moja ya nchi za Afrika Mashariki ambazo hazikosi matukio ya ajabu kila mara. Hii imetokea kwenye mji wa Eldoret ambapo kuna watu wanne walikamatwa wakifukua makaburi yaliyozikwa watu kuanzia wiki moja ili kuchukua vitu vya thamani walivyozikwa navyo.
Inaelezwa kuwa hiyo ni mbinu mpya ambayo imegunduliwa na wezi nchini Kenya inapotokea mtu amefariki basi wezi huwa wanakwenda mpaka kwenye mazishi na wanashiriki kama jamaa wa karibu ili tu kushuhudia marahemu amevalishwa au kuwekewa nini kwenye jeneza lake na kisha hurudi baada ya wiki moja kwaajili ya kubomoa na kuchukua vitu alivyozikwa navyo marehemu.
Matukio ya kuvunjwa makaburi yaliwashtua wakazi na ndugu wa karibu wa marehemu na kuamua kuweka lindo ili kuona watu wanaoyavunja ambapo walifanikiwa kuwakamata watu hao wakiwa wameshavunja kaburi moja na mmoja wapo akiwa ndani ya kaburi kitendo kilichopelekea watu hao kuwapiga na kutaka kuwafukia kwenye kaburi lililovunjwa.
Unaweza kutazama hapa chini kuona kilichotokea. Bonyeza Play

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.