Header Ads

Wolper Avuta Ndinga Ya Milioni 20Staa wa filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper amenunua gari lenye thamani ya shilingi milioni 20 ambalo kwa sasa anamalizia usajili wake

Ijumaa lilimbabatiza Wolper mitaa ya Kinondoni jijini Dar akiwa na gari hilo aina ya Toyota Alphard ambapo alipobanwa kama amelikodi kama wanavyofanya mastaa wengine au amenunua alifunguka kuwa ni lake kutoka kwenye hela yake halali.


 “Hii gari ni yangu kama mnavyoiona mpya kabisa, nimeinunua na ndo’ kwanza nashughulikia usajili,” alisema Wolper.

Wolper alisema kuwa anakwepa mambo yaliyompata kwenye ile gari yake iliyomletea matatizo aina ya BMW X-6 ambapo alipata funzo na sasa hawezi kufanya makosa


“Nimeamua nifanye usajili kabisa TRA, sitaki matatizo kabisa kuhusu magari, lile lilinifanya nipate funzo kubwa,” alisema Wolper.


Wolper mbali na kununua gari amefungua duka la nguo Kinondoni. Kufuatia mambo hayo makubwa aliyofanya msanii huyo, wadau walihoji kama mkwanja wa kufanyia yote hayo umetokana na safari ya China au kuna pedeshee kaamua kumpa maisha? Jibu analo mwenyewe.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.