Header Ads

AJALI MBAYA YA DALADALA NA LORI WATU KADHAA WAHOFIA KUPOTEZA MAISHA


Daladala baada ya kupata ajali.
Habari nilizozipata ni kwamba kuna ajali mbaya imetokea eneo la Tanangozi, Iringa. Hiace iliyokuwa inatoka Iringa mjini kwenda Ifunda imegongwa na lori lilokuwa limefeli break. Kuna taarifa za vifo vya watu zaidi ya nane.
Lori la mizigo lililosababisha ajali baada ya kupata hitilafu kwenye mfumo wa breki
Kwa taarifa zaidi naomba mliopo eneo hilo mtupatie.
Update
"Watu zaidi ya 20 waliokuwa wakisafiri na Hiace ya Iringa mjini Kwenda Ulete Iringa vijijini mkoani Iringa wamehofiwa kufa baada ya Hiace hiyo kugongwa na lori na kufunikwaTaarifa ambazo zimepatikana zinadai kuwa ajali hiyo imetokea majira ya saa 12 jioni wakati Hiace hiyo ikitoka Iringa kwenda Ulete na Lori likitokea Mafinga kuelekea Iringa mjini na kuwa ni dereva pekee wa Hiace ndie kapona na kukimbizwa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa.
Chanzo: Matukio Daima"

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.