Header Ads

DOGO Janja Afiwa na Baba yake


Msanii wa muziki wa hip hop kutoka Tip Top Connection Dogo Janja amefiwa na baba yake mzazi, Abubakari Chande.

Mzazi wake huyo ambaye alikuwa akiishi mkoani Arusha, ni mmoja kati ya watu wake wa karibu ambao walikuwa wanamshauri katika muziki wake.

Kupitia instagram, Dogo Janja ameandika:
PUMZIKA KWA AMANI BABA YANGU KIPENZI.😭 Hakika MUNGU Amefanya Maamuzi Yake Siwezi Kukufuru Zaidi Ya Kukuombea kwa ALLAH akupe kauli Thebeet! Umelala baba yangu sitakuona tena😭 EEH MWENYEZI MUNGU UMPOKEE,UMUONDOLEE ADHABU ZA KABURI. Lala baba hakika wote njia yetu ni moja.. siku moja tutaonana tena baba! R.I.P Kamanda ABUBAKARI CHENDE!
Kiongozi wa Tip Top Connection, Babu Tale amempa pole rapa huyo.

“Pole Dogo Janja Mungu akutie nguvu katika kipindi hiki kigumu na amuweke Baba katika njia inayo stahiki,” aliandika Babu Tale instagram.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.