Powered by Blogger.
[4] [Tech] [slider-top] [Technology]

Latest Post

HABARI KALI ZA WIKI

[15] [recent] [slider-top] [HABARI KALI ZA WIKI]

Technology

Lifestyle

HABARI ZA BURUDANI

[4] [burudani] [recent] [HABARI ZA BURUDANI]

Sports

VIDEO KALI ZA WIKI

NEW SONG:DIAMOND FT A,K,A

Gallery

Random Posts

Business

Boss Ngasa

Boss Ngasa

Video Of Day

STORI KALI ZA WIKI

[5] [habarimbalimbali] [recent] [STORI KALI ZA WIKI]

Popular Posts

Pages

STAY CONNECTED

[10] [recent] [slider-top-big] [HABARI KALI ZA WIKI]

CONTACT US

SIASA

[4] [siasa] [recent] [HABARI ZA SIASA]

Flicker Images

TUMA UDAKU PICHA AU VIDEO KUPITIA 0716909567

Facebook

About US

Advertisements

Entertainment

Follow US

You are here: Home / INASHANGAZA NA KUSIKITISHA BWANA Harusi Aliyekimbia Siku ya Ndoa Arudi Nyumbani

INASHANGAZA NA KUSIKITISHA BWANA Harusi Aliyekimbia Siku ya Ndoa Arudi Nyumbani

| No comment


Mbeya. Bwana harusi, Samuel Mwakalobo aliyetoweka muda mfupi kabla ya kufunga ndoa na Given Mgaya katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Isanga jijini hapa, amerudi nyumbani kwao juzi.

Kaka wa bwana harusi huyo, Braison Mwandemele ambaye ndiye aliyemlea, alisema alirudi nyumbani akiwa salama, lakini amepumzishwa bila kuulizwa lolote.


“Sijaongea naye lolote, yupo kwenye mapumziko, hivyo tunaomba mtuache kwanza,’’ Mwandemele alisema jana.


Mwakalobo (26) alizua taharuki Ijumaa ya Desemba 16, baada ya kutoonekana kanisani kufunga ndoa mbele ya Mchungaji Andagile Mwakijungu.


Kuhusu tukio hilo, Mchungaji Mwakijungu alisema ni la aina yake na linahitaji maombezi wala siyo kuzungumzazungumza ovyo.


Alisema aliitangaza ndoa hiyo siku 21 kanisani hapo kwa mujibu wa sheria na hapakuwa na pingamizi lolote na kwamba Alhamisi jioni (siku moja kabla ya harusi) alikutana wanandoa watarajiwa wote wawili na kuzungumza nao huku kila mmoja akiwa ni mwenye furaha na wakipeana miadi ya kuwahi ili wamalize mapema shughuli ya kuwaunganisha kimwili.


Mchunganji huyo alisema baada ya kuona tukio hilo limechukua sura mpya, alimuuliza bibi harusi kama kuna shida yoyote iliyojitokeza na kujibiwa kwamba hapakuwa na jambo lolote na kwamba hata yeye alishangaa kutomuona bwana wake wakati ndiye aliyempa hata fedha ya kwenda saluni.

MANGE KIMAMBI ACHOMA MOTO KADI YA CCM