Header Ads

https://www.youtube.com/channel/UCERjz5nmYNOtG_WBi-1S4xA

MAPENZO yangu na Jacqueline Wolper yapo Moyoni – Harmonize


Msanii wa muziki kutoka WCB, Harmonize amekanusha kuachana na mpenzi wake Jacqueline Wolper baada ya hivi karibuni kuzagaa taarifa katika mitandao ya kijamii kuwa wawili hao wameachana.

Madai hayo yalichukua sura mpya wiki chache zilizopita baada ya malkia huyo wa filamu kudaiwa kufuta picha za mkali huo wa wimbo Bado katika mtandao wake wa instagram.

Akiongea jana katika kipindi cha XXL cha Clouds FM, Harmonize alidai mapenzi yao yapo moyoni na watu wasichanganywe na issue ya kufuta picha instagram.

“Wolper alifuta tu picha za instagram hakufuta mapenzi yetu yapo moyoni,” alisema Harmonize.

Pia muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo Matatizo, alidai suala la malkia huyo kufuta picha instagram ni kawaida kwani anaweza kufuta na kuanza kupost mpya.

Wapenzi hao wamebadili utaratibu wa maisha yao kwani huko nyuma walikuwa wanasafiri na kula bata pamoja.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.