Header Ads

MATARAJIO Makubwa ya Kupata Kazi Baada ya Masomo, Yanatuponza - stuffzoom


Ni kweli kwamba tunapokuwa vyuoni au tunapopata nafasi za kujiunga na vyuo wengi wetu matarajio ni kumaliza na kuja kupata kazi nzuri zenye mishahara minono minono.

Ila matarajio huwa sio pale tunapomaliza vyuo na kukuta tunamaliza siku, miezi, miaka bila kupata kazi. Huwa inakatisha tamaa sana kwani hapo mwanzo matarajio yalikuwa makubwa sana na wengine huamua tu hata kuendelea na masomo ya juu kama uwezo upo huku wakiwa wanaendelea kutafuta kazi taratibu, au hata kuta tamaa kabisa na keundelea na mambo mengine.

Kuna namna ambavyo elimu yetu ya Tanzania inashindwa kuwatengeneza watu wakiwa bado vyuoni au masomoni, wanashindwa kutengeneza watu kukabiliana na wakati uliopo, na changamoto zake. Wanashindwa kutengeza watu kutotegemea ajira tu na kufikiria vitu vingine kama kujiajiri na kuwa wabunifu. Elimu yetu ni bado ile ya kukremishwa na misingi yake haina mashiko na maisha halisi ambayo mlengwa atakuja kupitia baada ya masomo yake, Hivyo hili ni tatizo kubwa sana na linahitaji ufumbuzi wa haraka.

Ushauri kwa serikali, Mfumo wa elimu yetu ya Tanzania unabidi kuangaliwa tena upya, kuna haja ya kubadilisha namna ya ufundishaji, uwe wa maisha halisi zaidi na kwenda na wakati, zama zina badilika kila siku lakini mitaala ni ile ile ya miaka hamsini iliyopita. Hakuna ubunifu kwenye baadhi ya mafunzo. Watu wanabidi wapewe elimu za kujitegeme na sio Kutegemea ili kuepusha "Disappointment" Baadae

Hapo chini ni njia chache unazoweza kutumia kupata ajira mpya, au kupata ajira bora zaidi

1. Sasa hivi sio muda wa kusoma tu course kwasababu unaipenda, soma kitu adimu, chenye soko kwenye ajira, Ajira ni ushindani kwasasa, hivyo ilikushinda lazima uwe na kitu ambacho wengi hawana.

2. Usichoke hata mara moja kutafuta kazi, na wala usivunjike moyo kama umeshaitwa kwenye interviews kadhaa na haziku zaa matunda, jua kwamba unavyofanya interviews nyingi zaidi zinakujenga na kukupa ujasiri zaidi na pia kujua makosa yako na kujirekebisha.

3. Omba kazi ambayo unaona unafiti, kulingana na elimu yako na ujuzi. Usiombe tu kazi kwasababu umeona Tangazo, na hiki ndio chanzo wakati mwengine chakutuma maombi mengi yasiyo na mafanikio.

4. Tengeneza Connections Zenye Faida, chati pia wasiliana na walio kutangulia kupata kazi, Maana Kazi nyingi siku hizi zinatangazwa ndani kwani ndani (internally) na ndio mana kuna makampuni huwezi kuona popote wametangaza kazi, Lakini wanaajiri .

5. Usidharau mitandao kazi nyingi hutangazwa Mitandaoni siku hizi, achana na zama za zamani za magazeti, Tembelea mitandao tofauti kama >> http://stuffzoom.com/

Nakutakia kila la Heri kwenye Pilika za Maisha - Stuffzoom

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.