Header Ads

https://www.youtube.com/channel/UCERjz5nmYNOtG_WBi-1S4xA

MKE WA MTU SUMU:DEREVA Bodaboda Akatwa Sikio Kwa Tuhuma ya Kufumaniwa na Mke wa Dereva Teksi


Dereva bodaboda wa Mji Mdogo wa Qatesh wilayani Hanang’ Mkoa wa Manyara, amekatwa sikio kwa kisu kwa tuhuma za kufumaniwa akiwa na mke wa dereva wa teksi.


Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Manyara, Kamishna Msaidizi, Francis Massawe alisema tukio hilo lilitokea Desemba 21 saa 6:10 usiku kwenye Kitongoji cha Qendangonyi, Kata ya Ganana wilayani Hanang’.

Kamanda Massawe alisema chanzo cha tukio hilo ni wivu wa mapenzi na majeruhi amepata kilema cha maisha baada ya sikio kutolewa.

Alisema wanamshikilia dereva teksi kwa uchunguzi wa tukio hilo kabla ya kumfikisha mahakamani.

Source: Mwananchi

KIJANA AELEZEA JINSI ALIVYORUBUNIWA NA MAMA MCHUNGAJI WAFANYA MAPENZI YouTube

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.