Header Ads

MWANA FA Asema Wimbo "Muziki" wa Darassa Umerudisha Heshima Kwa Wasanii wa Hip Hop


Msanii wa muziki wa hip hop, Mwana FA amesema hatua ya mafanikio ya wimbo ‘Muziki’ wa Darassa ni hatua ambayo wasanii wengi wa muziki wa hip hop walishindwa kuifikia kwa muda mrefu.
Rapa huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo wake ‘Dume Suruali’ amesema ni muda mrefu wasanii wa hip hop walikuwa wanashindwa kutoa ngoma ambazo zitaleta ushindani mkubwa na zawasanii wa kuimba.

“Kwanza I’m happy for rap music,” FA alikiambia kipindi cha FNL cha EATV. “Imekuwa muda mrefu hatujawahi kutengeneza nyimbo halafu zikatoka na nyimbo za waimbaji, halafu usisikie nyimbo za waimbaji na rap music ikawa vile,”

Mwana FA amesema anapenda kuona Darassa akiendelea kufanikiwa zaidi katika muziki kwa kuwa ni msanii ambaye anaujua uwezo wake katika kile anachokifanya.

Wimbo ‘Muziki’ wa Darassa umeweza kufanya vizuri kwenye chart mbalimbali za muziki. Pia kupitia channel ya mtandao wa YouTbe video ya wimbo huo imeweza kuangaliwa mara 1,787,074 katika kipindi cha wiki tatu.


VIDEO:Watu wamzushia Kifo WEMA SEPETU SIKIA AKIKANUSHA

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.