Header Ads

https://www.youtube.com/channel/UCERjz5nmYNOtG_WBi-1S4xA

Duh:Umesiki Hii ya Vanessa Mdee Juu ya Kuigiza Tamthiliya ya Mtv Shuga,Sasa Soma Hapa Kujua Mtonyo Anaobeba Kwa kila Epsode

vanessa-mdee-3
KABLA ya mwanzoni mwa Machi, 2013 mwanadada mwenye asili ya Kenya na muigizaji mahiri duniani, Lupita Nyongo hajatangazwa na mchekeshaji Will Smith mjini Los Angeles, Marekani kuwa ndiye mshindi wa Tuzo ya Oscar kupitia kwenye filamu yenye maudhui ya utumwa iitwayo 12 Years A Slave, iko wazi ni watu wachache waliokuwa wanamfuatilia duniani.

Huo ndiyo ukweli halisi maana hata vyombo vya habari vimeanza kumuandika zaidi baada ya tuzo hiyo. Hata hivyo kiuhalisia si kwamba filamu hiyo iliyompa tuzo akiwa Muigizaji Bora Msaidizi wa Kike ndiyo ya kwanza kwake kufanya.

Ameonekana kwenye filamu nyingi na michezo ya jukwaani mbalimbali ikiwemo The Winter’s Tale, Lights, Chekhov’s Uncle Vanya na The Taming Of The Shrew ulioandaliwa na mwandishi maarufu duniani William Shakespeare.
Hata hivyo mbali na michezo hiyo pia Lupita Nyongo alitikisa kwenye tamthilia ya MTV iitwayo MTV Shuga kwenye msimu wa kwanza, tamthilia ambayo mwanadada kutoka Bongo, ambaye ni mwanamuziki mwenye ‘fun base’ kubwa Afrika kwa sasa, Vannesa Mdee ‘Vee Money’ au  Cash Madame amepata shavu la kuuza sura katika msimu wa tano. Jambo linalokamilisha usemi kuwa anapasua mulemule alimopita Lupita Nyongo.
vanessa-mdee-2 Showbiz: Katika makala hii, Vee Money akifanya mahojiano na Uwazi Showbiz, anaelezea kwa upana ‘career’ yake hiyo mpyaUmepata shavu la kuuza sura kwenye tamthilia, hebu elezea kinagaubaga, tamthilia inaitwaje na ilikuwaje ukapata mchongo huo?
Vee Money: Ni Tamthilia ya MTV inaitwa MTV Shuga. Huu ni msimu wao wa 5. Nilipata kazi kwa kufanya ‘audition’ baada ya wao wenyewe kuniomba nifanye hivyo.
Showbiz: Baada ya kupita kwenye audition, ni ugumu gani umekutana nao lokesheni na ni tofauti kabisa na kushuti video za muziki?
Vee Money: Hakuna ugumu wowote labda tu kumeza script. Ni kazi ngumu lakini kwa kuwa nimeamua kufanya, inabidi kukomaa.
Showbiz: Vipi kuhusu nafasi uliyopewa kucheza, imeendana na wewe na umeifurahia?
Vee Money: Kiukweli kwenye ‘character’ pia kulikuwa na changamoto kwa sababu aina ya mwanadada niliyetakiwa kucheza, siendani naye kabisa, lakini kwa kuwa ni kazi ya sanaa haikuwa na budi kufanya kila nililotakiwa kufanya ilimradi tu kuitendea haki nafasi hiyo.
Actress Lupita Nyong'o, of the film "12 Years A Slave," arrives at the 71st annual Golden Globe Awards in Beverly Hills, California January 12, 2014. REUTERS/Mario Anzuoni (UNITED STATES - Tags: ENTERTAINMENT) (GOLDENGLOBES-ARRIVALS) - RTX17B4R

                                                                      
Showbiz: Tamthilia hii inafanyikia wapi?
Vee Money: Johannesburg, South Africa
Showbiz: Unatumia muda gani kukaa lokesheni?
Vee Money: Nakaa siku kumi lokesheni. Lakini pia kila baada ya wiki mbili ninakuwa naenda maana tamthilia yenyewe itatoka April.
Showbiz: Umegundua nini tofauti kati ya uandaaji wa filamu na tamthilia za Kibongo na nje?
Vee Money: Sijawahi kushiriki kutengeneza filamu za nyumbani, kwa hiyo sifahamu lolote, lakini wenzetu nje wanajipanga sana.
Showbiz: Ni waigizaji gani wengine maarufu ambao umeigiza nao?
Vee Money: Wapo wengi, kutoka Afrika Kusini na Nigeria, siwezi ila kuwataja kwa majina.
Showbiz: Kuhusu malipo vipi, unaweza kuzungumzia lolote?
Vee Money: Kikubwa ni kwamba kila ninapokwenda wananiita Cash Madame, so hata kama ni malipo ni ya kuridhisha tu.
 Showbiz: Kabla ya kupata nafasi hii, uliwahi kuwaza siku moja kuwa utakuwa muigizaji?
Vee Money: Ndiyo, ni ndoto zangu za muda mrefu sana, so namshukuru Mungu amenionyesha mlango nategemea kufanya zaidi ya hiki ninachokifanya.
Showbiz: Ni muigizaji gani unamkubali zaidi duniani?
Vee Money: Viola Davis
Showbiz: Nini mipango yako zaidi kuhusu muvi na tamthilia?
Vee Money: Nitaweka wazi wakati ukifika.
Showbiz: Kipi ambacho unapenda Watanzania wakifahamu ambacho sijakuuliza.
Vee Money: Hii tamthilia ndiyo ilimtoa Lupita Nyongo, aliigiza kwenye msimu wa kwanza, kwa hiyo mimi pia wategemee mambo makubwa sana.
Showbiz: Nakushukuru kwa ushirikiano Cash Madame na kila la kheli katika ‘keria’ yako.
Vee Money: Asante

Maiti yakutwa chumbani saa chache baada ya kuzikwa makaburini MBEYA

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.