Header Ads

INASHANGAZA SANA.HAYA NDIO MAAJABU YALIYOMTOKEA DARASSA HUKO KIGOMA,

Wiki iliyopita team nzima ya XXL ya Clouds FM ilijisogeza pande za Kigoma kama mwanzo wa mipango yao kwa mwaka huu ya kufanya XXL Tour kwa jumla ya mikoa 12 hadi mwaka huu unaisha, ikiwa ni tukio la kila mwezi linalo ambatana na kumtangaza msanii bora wa mwezi.

Ambapo kwa mwezi huu wa kwanza Darassa CMG aliweza kudondokewa na shavu hilo na kuweza kukwea mwewe mpaka pande za Kigoma ambapo ndio mkoa wa kwanza kufanyika kwa tukio hilo la XXL Tour.
Ni love ya kutosha ambayo wana Kigoma waliionyesha kwa team hiyo kuanzia kwenye mapokezi mpaka kwenye uitikiaji wa matukio ambayo yaliipeleka team hiyo pande hizo.
Suala la mapokezi haikuwa issue kwa Darassa, bali Darassa amefunguka kitu ambacho kilim-surprise pande hizo za Kigoma.
“Mapokeo ambayo nimepokelewa haikuwa surprise kwasababu salamu zilikuwa zinanifikia za kuitwa Kigoma siku nyingi lakini ratiba tu zilikuwa zinanibana. kitu ambacho nimekuja kukipenda ni jinsi ambavyo Kigoma inaweza kuendesha mambo yake, kuna kila kitu cha kuweza kufanya Kigoma iko full kwasababu nimeona kuna ziwa na kuna nyenzo kubwa ambayo maji yanaweza yasiwe tatuzo kwa muda mrefu, so inawatengenezea mazingira mazuri watu wa Kigoma kuweza kufanya shughuli nyingi sana”

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.