Header Ads

Kudadeki..!!Kanisa la Anglikana Lamwandalia Adhabu Kali Askofu Mokiwa kwa Kuwa Mkaidi..!!!!

Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana nchini, Jacob Chimeledya amesema watachukua hatua zaidi dhidi ya Askofu Valentino Mokiwa wa kanisa hilo Dayosisi ya Dar es Salaam kwa kuwa bado anaendelea kutoa huduma licha ya kutakiwa kujiuzulu.

Wiki tatu zilizopita Mokiwa aliandikiwa barua na Askofu Chimeledya akitakiwa kujiuzulu akidaiwa kuvunja miiko ya kanisa hilo na kutumia madaraka yake vibaya ikiwamo kufanya ubadhirifu wa fedha.

Hata hivyo, Dk Mokiwa amekuwa akikana tuhuma dhidi yake akisema mgogoro wa kanisa hilo ni wa kutengenezwa na adui zake.

Akizungumza kwa simu na Mwananchi jana, Askofu Chimeledya hakuzitaja hatua zitakazochukuliwa dhidi ya Askofu Mokiwa, akisema hakuna ulazima wa kuziweka hadharani hadi pale zitakapochukuliwa na kanisa hilo.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.