Header Ads

Mwanaume Ataka Kumlipa Mungu Pesa Ili Amsamehe Dhambi zake...Azikwa na Dola Elfu Tano


Charles Obong alitaka kumlimpa Mungu ili ampe msamaha kwa dhambi zake
Mwanamume mmoja nchini Uganda amezikwa pamoja na dola 5,700 pesa taslim, ambazo alitaka kumlimpa Mungu ili ampe msamaha kwa dhambi zake na kumuokoa kutoka kwa moto wa ahera.
Charles Obong, mfanyakazi wa zamani wa serikali ambaye aliaga dunia akiwa na umri wa miaka 52, aliomba hilo kwenye wosia wake, kwa mujibu wa familia yake.
Licha hiyo kutekelezwa, kaburi lake lilifukuliwa na pesa hizo kuondolewa kutoka wa jeneza lake, baada ya wazee wa jamii kufahamu kilichotokea, kwa mujibu wa gazeti la the Daily Monitor.
Gazeti hilo lilimnukuu askofu mmoja wa kiangilikana Joel Agel, akisema hakuna pesa zinazoweza kununu uzima wa milele na Mungu hawezia kupokea pesa kama malipo.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.