Header Ads

https://www.youtube.com/channel/UCERjz5nmYNOtG_WBi-1S4xA

Oh Nooh!! Mamilioni ya Mtoto wa Pili wa Diamond Yatoweka Kimiujiza,Mwenyewe Asema Hilo Halimsumbui..!!

diamond
Diamondakiwa amembeba mwanaye mchanga, Nillan.
Matarajio ya mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ya kumtumia mwanaye Nillan kupata mamilioni ya pesa kutoka kwa wadhamini yanadaiwa kubuma kufuatia maelezo kuwa, baadhi ya makampuni yaliyokuwa yamezungumza naye yameamua kujiweka pembeni kutokana na ukata wa pesa.

Awali, akizungumza  hivi karibuni, Diamond aliweka wazi kuwa, kabla hata mtoto hajazaliwa kuna benki mbili ambazo zilimwaga dau la mamilioni ya pesa kwa ajili ya kutumia picha ya mtoto huyo kwenye huduma zao lakini yeye alikuwa hajaweka wazi ipi aingie nayo mkataba na kwa mkwanja upi.
Diamondakiwa amembeba mwanaye mchanga, Nillan.
Hata hivyo wakati mtoto huyo akikaribia kufikisha mwezi mmoja, taarifa zilizotufikia zinadai kwamba baadhi ya makampuni yaliyojitutumua kutaka kutoa mamilioni kwa ajili ya sura ya mtoto huyo yameingia mitini.
Chanzo makini kilicho karibu na msanii huyo kilidai kuwa, awali Diamond alikuwa amefanya mazungumzo na makampuni na mabenki tofauti lakini kutokana na hali ngumu, baadhi wamekaa kimya mpaka sasa.
“Kimsingi yale mamilioni ambayo Diamond na Zari walitarajia kuyapata kutoka kwa makampuni na benki kama ilivyokuwa kwa Tiffah, yamebuma. Mambo yamekuwa siyo.
“Inavyoonekana huku kubana pesa za dili kwa Rais John Magufuli kumewafanya hata wale waliokuwa wakitaka kutoa pesa ili wanunue sura ya Nillan wafanye uamuzi wa kupotezea.”
zari-na-mond-kidZari (aliyelala) ikiwa ni saa chache baadea ya kujifungua
Umaarufu wa Nillan umechangia?
Aidha, wachambuzi wa mambo wameeleza kuwa, kubuma kwa mapesa hayo kunaweza kuwa kumetokana na mtoto huyo kutovuma kama ilivyokuwa Tiffah hivyo kuna ambao wameona kutoa pesa kwa ajili ya sura yake ni sawa na kuzitupa.
“Kipindi cha Tiffah ilikuwa rahisi sana benki na makampuni mbalimbali kutoa pesa ili kununua sura yake kwa kuwa alikuwa ‘hot’ na pia fedha ilikuwa inapatikana kirahisi lakini ikimbukwe huu ni utawala na Magu, pesa haitoki kirahisi.
“Pia Nillan mpaka sasa hawezi kuishawishi benki yoyote itoe mamilioni kununua sura yake kwa kuwa hana kiki kivile. Kwa mfano Tiffah alipozaliwa na kufunguliwa ukurasa wake wa Insta, ndani ya siku mbili tu alikuwa na followers (wafuasi) 200,000 lakini kwa Nillan akiwa anakaribia kufikisha mwezi mmoja ana followers 69,000, hiyo inaonesha watu hawamshobokei na hata kibiashara sura yake haiwezi kuwa kivile,” alisema Rashid Maguli wa Kinondoni ambaye ni shabiki mkubwa wa Diamond.
zari-na-diamondDiamond na mpenzi wake, Zari
Hili linaweza kutokea pia
Ikazidi kudaiwa kuwa, kuna uwezekano kwa mara ya kwanza Diamond akaamua kuionesha picha ya Nillan bila kuwa na mdhamini au akapata wadhamini lakini akapewa ‘pesa mbuzi’ tofauti na matarajio yake.
Diamond anasemaje?
Kufuatia kumwagika kwa ubuyu huo, paparazi wetu alifanya jitihada za kumtafuta Diamond ambapo alipopatikana alisema hawezi kulizungumzia suala hilo kwa kirefu kwa kuwa bado mazungumzo yanaendelea na anaamini kila kitu kitaenda sawa.
“Kila kitu kinaenda sawa, niliongea na baadhi ya wadhamini na kuwaambia wasubiri mtoto azaliwe, sasa amezaliwa naamini kila kitu kitaenda sawa, hayo mambo ya kubuma siyajui,” alisema Diamond.
Tujikumbushe kidogo
Mwaka jana, Agosti 6, Tiffah alizaliwa na siku chache baadaye akalamba mkataba mnono wa Ubalozi wa Benki ya NMB na maduka makubwa ya vitu vya watoto.

No comments:

Powered by Blogger.