Header Ads

Ajali ya Gari Yaua Saba Wakiwamo Viongozi wa CCM na Mwanahabari KilimanjaroKILIMANJARO: Watu saba wamefariki dunia wakiwemo Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Hai, MNEC wa Wilaya ya Same pamoja na mwandishi mmoja wa Gazeti la Habari Leo Bw. Anold Swai, baada ya gari waliokuwa wakisafiria kupata ajali ya kugongwa na Fuso la mizigo katika eneo la Mwika Mawanjeni Maarufu kama Bar Mpya mkoani Kilimanjaro.
Ajali hiyo imetokea leo majira ya saa 11 jioni baada ya gari aina ya Fuso lenye namba za usajili T 343 BNL lililokuwa limebeba mizigo ya ndizi likitoka Rombo kuelekea Dar es Salaam, kuligonga gari dogo aina ya Toyota Surf lililokuwa likitokea Mkuu Rombo kwenda Moshi.
Aidha mbali na kugonga gari hilo dogo, fuso hilo limegonga pikipiki aina ya MT 131 ANC, King Lion ambayo ni boda boda iliyokuwa ikitoka Mwika kwenda Himo. Polisi Mkoani Kilimanjaro wamethibitisha.
Katika ajali hiyo kumeripotiwa majheruhi wawili ambao wamepelekwa katika Hospitali ya KCMC kwa ajili ya uchunguzi na matibabu huku miili ya marehemu ikipelekwa hospitalini hapo kwa ajili ya kuhifadhiwa.
Taarifa za awali zimeeleza kuwa msafara huo ulikuwa ni wa viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliokuwa wakitoka kwenye sherehe za kuadhimisha miaka 40 tangu kuzaliwa kwa chama hicho, sherehe ambazo zilifanyika Kimkoa wialayani Rombo.
Imeelezwa kuwa gari walilokuwa wakisafiria ambalo limepata ajali lilikuwa ni la MNEC wa Same ambaye pia amepoteza maisha kwenye ajali hiyo huku idadi ya majeruhi ikiwa haifahamiki.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.