Header Ads

Askari 12 Waliotuhumiwa Kushirikiana na Wauza Unga Wasimamishwa Kazi


Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Ernest Mangu amewasimamisha kazi askari 12 waliotuhumiwa kujihusisha na madawa ya kulevya wakati uchunguzi ukiendelea.

IGP huyo amewaambia wanahabari, Jumamosi hii katika makao makuu ya Polisi huku akisema kuwa Polisi ndiyo chombo kinachoongoza mapambano juu ya madawa hayo, huku akisema kuwa hatua zitachukuliwa dhidi ya askari atakayetuhumiwa.

“Tumeamua kuwasimamisha kazi wote walioguswa moja kwa moja na sakata hili, pia Polisi itachukua hatua madhubuti ikiwemo kuwapeleka mahakamani wasanii waliotuhumiwa,” alisema.

Askari hao ni wale waliotajwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda siku mbili zilizopita wakati akiwaambia wanahabari juu ya watu wanaotuhumiwa kujihusisha na biashara na matumizi ya madawa hayo.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.