Header Ads

Mwanamke Ambae Natarajia Kumuoa Miezi 4 Ijayo Ananisaliti...Ushauri Wahitajika


Habari watanzania wenzangu
Nianze moja kwa moja kuna mkasa umenifika kama mwanaume ninayetarajia kufunga ndoa miezi minne ijayo lakini imetokea sintofahamu kubwa cn kwa mwenzangu kubadilika mm
Nafanya kazi dar na yy mkoani. mwenzangu katokea kubadilika kabisa ni ugomvi usioisha mpaka imefikia hatua tunashindwa kupanga vitu kuhusiana na ndoa yetu. Pia mahari kila kitu nilishatoa na mpaka ss hv pande zote mbili zinaendelea na vikao vy shughuri.

Mabadiliko haya yametokea gafla bila hata kutibuana wala kugombana ila kutokana na upelelezi hakinifu nimekuja kujuwa kaanza mahusiano na jamaa mmoja anafanya naye kazi nimefatilia kupitia system nilizonazo za cm za kila kitu nimejuwa kuwa ananisaliti na mpaka tarehe ya kunisaliti naijuwa kanisaliti tarehe 30 /1/2017 muda wa saa 4 usiku na pia tarehe 31/1/2017 tena kanisaliti muda kuanzia saa 3 usiku kalala kwa hyo jamaa
Imeniumiza sana nikifikiria kwa sasa tulipo hiki kitu kinatokea naumia naenda kazini sio mimi nimejaribu kutaka kuchukua maamuzi mazito moyo unasita najaribu kuuliza watu kupitia indirect way wanajibu inatakiwa kuwa na subira na kuwa na uvumilivu sana ila inauma sana.

Wanandugu naombeni ushauri nifanyeje kuhusiana na hili swala kwani nikiwa peke yangu nawaza sana inanibidi nijichanganye kupiga story kwa sana ili nijisahaulishe lakini jaman naomba ushauri nifanyeje
samahani kama nitakuwa nimewaudhimnisamehe.
Ni mm mwajamii mwenzenu.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.