Header Ads

RC PAUL MAKONDA ATAJA LIST YINGINE YA MAJINA MAPYA WATUHUMIWA WA DAWA ZA KULEVYA


DAR ES SALAAM: Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amemtaja na msanii wa Bongo Fleva, Vanesa Mdee ‘Vee Money‘ kuwa ni miongoni
mwa wanaotuhumiwa kuhusika na mtandao wa biashara haramu ya madawa ya kulevya baada ya jina lake kuongezwa kwenye orodha iliyotajwa jana .
Makonda ameyasema hayo leo wakati akizungumza na wanahabari wakati akitoa taarifa kuhusu kuitikia wito kwa wasanii 9 na askari polisi aliowataja jana kuhusika na biashara hiyo. Aidha Makonda amemtaka Vee Money kuripoti katika Kituo hicho Jumatatu ijayo kwa ajili ya mahojiano zaidi. Taarifa hiyo ilitolewa na Makonda katika ofisi ya Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es salaam, Kamishana Sirro, iliyopo sentro.
Makonda ameeleza kuwa ni watu watano tu ambao ni wasanii na raia wa kawaida ndiyo wameripoti leo kati ya wale waliotajwa jana. Mbali na hivyo, Makonda ametoa agizo kwa polisi kuwa, wale ambao hawajaripoti, watafutwe na wakamatwe hadi kufikia Jumatatu.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.