Header Ads

Wema Sepetu, Asiyefunzwa na Mamaye Hufunzwa na Ulimwengu..!!!


Nakumbuka miaka ya zamani lulu nae alikua hivi hivi hashikiki, kila club yeye, kila rafiki yeye, mtoto alikua hashikiki mpaka mama yake akainua mikono, lulu anatoroka kwao usiku wa manane anaenda kwa wanaume, maisha yake yalikua kwa mashosti, shule akaikacha, umaarufu ukampa kichwa akajiona yeye ndio yeye, siku ya siku ikatokea ajali ( wote mnajua yaliyotokea) akawekwa rumande miezi kadhaa, Lulu akawa lulu machozi, alikonda ,maisha yake kila siku vilio, mashost wote wakamkacha, hakuna aliyekua na habari nae alipokua rumande, kila mtu alimkashifu kwa style yake, lulu akawa lulu machozi, rafiki yake akawa BIBLIA na rosali, lulu akamgeukia Mungu, Mungu si athumani akasikia kilio chake akatoka kwa dhamana, akawa HURU, tokea hapo hatukuwahi kumsikia lulu na marafiki wa ajabu ajabu, lulu club akawa haonekani,familia yake ndo ikawa rafiki yake pamoja na muna love na baadhi ya mastaa wachache, sasa hivi huwezi kukuta picha za lulu akilewa hovyo kama zamani (kuna tetesi aliacha pombe) , lulu akabadilika kabisa akawa mpya, sasa hivi katulia na boyfriend wake.
Back to wema, nadhani ni wakati wa mashabiki wa wema waache kushabikia upuuzi, hivi karibuni wema amekua na scandal chafu za kubadili wanaume na kuongozana na mashoga wasio na focus na maisha, wema kampani yake wanaume mashoga, mashangingi na wauza madawa (pengine hii imemcost) inawezekana mdada wa watu hata hausiki ila kwa kuwa anaongozana na wezi na yeye lazima wamuhisi mwizi, nadhani hili litakua ni funzo kwake, mama yake kashalia sana na wema mpaka wamegombana ila wema hasikii,anaishi maisha anayotaka yeye, pengine ni hao hao marafiki zake wa karibu wamemchomea, MIMI NADHANI WEMA AKIWEKWA NDANI KAMA MIAKA MIWILI AU MITATU nadhani atabadilika, najua watu watafikiria vibaya ila SIO KILA JAMBO BAYA LINATOKEA KWENYE MAISHA YETU KWA NIA MBAYA,mengine yanatokea kama funzo au baraka, mi nadhani ni wakati wa wema kukubali matokeo na kukaa ndani, im telling you akitoka wema atakua anaimba GOSPEL, huruma zenu zitamponza, jela hapaui ni sehemu ya kujifunza.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.