Header Ads

Alichokisema Wabogojo Baada ya Kuoa ...!!!!

Mchekeshaji ambaye aliwahi kujizolea umaarufu mkubwa kwa kucheza kwenye nyimbo za msanii Mr. Nice enzi hizo Wabogojo jana ameuaga ukapela kwa kuvuta jiko ndani na kuachana na maisha ya u bachelor.
Wabogojo ambaye muda mwingi sasa amekuwa nje ya nchi baada ya kufanikiwa kufunga ndoa aliweza kuwashukuru ndugu jamaa na marafiki kwa kuweza kumpa support katika jambo hilo ambalo ni muhimu katika maisha yake. 
"Hatimaye ni mume na mke. Ahsante Mungu nimebarikiwa kwa jambo hili, familia yangu kwa ujumla sina cha kulipa kwa upendo wenu kwangu kwa jinsi mlivyoweza kuniunga mkono katika jambo hili, nawapenda sana wote marafiki, ndugu, wafanyakazi wenzangu, nashukuruni sana. Nashukuru sana mke wangu kwa kunikubali katika maisha yako kwa hivi nilivyo, nakupenda sana na upendo wangu kwako hauna mwisho" alisema Wabogojo 

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.