Header Ads

Amber Lulu Awafunda Wanaotafuta Umaarufu Mitandaoni


Mrembo anayepamba video za wasanii bongo ' Amber Lulu amewataka warembo wenzake kubadilisha mfumo wa maisha wa kutafuta umaarufu kupitia mitandao ya kijamii kwa kupiga picha zisizofaa na badala yake wafanye kazi za kusaidia jamii ili wakumbukwe.

Akipiga story kwenye  Planet Bongo Amber anasema amegundua kuwa kutumia sehemu za miili yao kutafuta umaarufu ni kitu kisicho na maana kwa kuwa umaarufu huo unakuja na kupita kitu ambacho mwisho wa siku watakuwa hawana kitu kipya cha kuonesha kwa mashabiki na kubaki kunyooshewa vidole kwa sababu ya picha hizo wanazotafutia kiki.

"Kutumia maungo kwa ajili ya kutafuta umaarufu siyo mpango kwa kuwa upepo huo utapita halafu tutakuwa hatuna cha kuonesha, bado watoto wa kike tuna mambo mengi ya kufanya kwenye jamii na tukaonekana kuliko kuonesha miili yetu ambapo mwisho wa siku tunadharaulika." Amesema Amber

Hii siyo mara ya kwanza video vixen huyo kufunguka suala la kuacha sehemu kubwa ya mwili wazi, Wiki iliyopita Ambar Lulu alisema umaarufu wa kuutafutia kwenye mitandao ya kijamii ni kama upepo kwani hutokea na kupita kwa kuwa warembo wapo wengi na kila mmoja anatafuta njia ya kutokea. 

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.