Header Ads

Bodaboda Washtukiwa Juu ya Tabia Zao za Kulala Kimapenzi na Wanafunzi wa Shule..!!!

Mkuu wa Dawati la Jinsia Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Dar es Salaam, Inspekta Prisca Komba amewaonya madereva bodaboda kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mabinti wa shule na badala yake wawe mstari wa mbele kulinda na kuwasaidia kutimiza malengo yao
Akizungumza leo ikiwa ni maadhimisho ya siku ya wanawake duniani kwenye kipindi cha East Africa Breakfast cha EA Radio, Inspekta Komba amesema katika dawati lake la jinsia kesi nyingi anazopata ni za madereva kuwapatia mimba wanafunzi na kisha kuwatelekeza kitu ambacho kinamuumiza zaidi ni pale binti anakuwa ammeachishwa shule na mwenye mimba anakuwa kakimbia
"Huwa naumia sana nikiwa napokea kesi za aina hii. Unajua hawa bodaboda siyo vijana wabaya lakini niwaambie kwamba, kama umempenda binti wa watu fuata njia sahihi za kumpata, siyo tena kumharibia masomo yake na mtoto umtelekeze maana hata wakati mwingine huwa hawasemi kweli wanapoishi, boda boda waacheni wanafunzi wasome.
Aidha Bi. Komba ameongeza kuwa licha ya kuhitaji mabinti walindwe kuepukana na mimba za utotoni lakini pia ameiomba jamii nzima kuhakikisha mtoto wa kike anathaminiwa kwa kupatiwa taulo za kujisitiri wakati wa hedhi hasa kwa wale wanafunzi wanaotoka katika mazingira magumu.
"Hili jambo hebu tusiachiwe wanawake tu kwa sababu lipo katika miili yetu. Kama mimi mwanamke mume wangu hatonithamini kwa kuninunulia vifaa vya kusitiria nikitumia vifaa vichafu nikipata magonjwa naye nitamuambukiza, kwa kuangalia hivyo hili jambo ni letu sote." Amesema Komba.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.