Header Ads

Ciara Anusurika Kupoteza Ujauzito Wake Kwenye Ajali Ya Gari – (Pichaz)


Staa wa muziki wa Marekani Ciara anusurika kupoteza ujauzito wake kwenye ajali ya gari jijini Los Angeles, mtandao wa TMZ umeripoti.
Ciara ambaye ni mjamzito wa miezi saba amenusurika kupoteza maisha yake na ya mtoto wake siku ya Ijumaa baada ya gari aina ya Volvo kugongana na Mercedes Benz yake uso kwa uso.
Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, hakuna aliyeumia kwenye ajali hiyo huku Page Six mtandao mwingine ukithibisha kile kilichosemwa na TMZ kwa kuachia statement ilyiotolewa na msemaji wa Ciara, ambapo msemaji huyo amesema:
Watu wawe na amani, Ciara na mtoto wote wapo sawa. Hali zao zinaendelea vizuri. Kilichotokea ni kwamba dereva aliyegongana na gari ya Ciara alikuwa anaendesha gari yake kwenye njia ya mabasi yaendayo kwa mwendokasi hivyo kusababisha kugongana na Ciara ambaye alikuwa amekaa upande sahihi wa barabara…” – Msemaji huyo aliiambia Page Six.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.